Ukiamua kutumia digital platforms kutangaza huduma/biashara yako ili watu wengi waifahamu, wakutafute ufanye nao kazi (partners), wanunue bidhaa zako n.k inahitaji kujitoa muda wako, pesa na kuwa tayari kuendana na hali ya soko.
Kutumia majukwaa ya mtandaoni kama vile mitandao ya kijamii na websites ni hatua muhimu kwa mafanikio ya biashara au huduma yako. Hii ni njia nzuri na rahisi ya kufanikisha malengo ya kuwafikia wateja au kupata washirikiana wapya (partners)
Kuanza Safari ya Kidigitali
Ili kufanikisha uwepo wa biashara yako mtandaoni unakuwa, hakikisha unajitosa kwa dhati kwa moyo wako wote ili ufikie kile unachotarajia. Kubali gharama za mwanzo kwani ni sehemu ya mchakato wa kujenga msingi imara wa biashara yako. Mwanzo mara nyingi huwa mgumu, lakini ni hatua muhimu kuelekea mafanikio ya muda mrefu.
Siku zote mtu anayefikiria mbali kuhusu biashara yake hujiulize maswali haya:
- Je, baada ya miaka 10 ijayo, wateja wangu watatumia njia gani kunifikia?
- Ni mikakati gani itakayorahisisha kufikia wateja hao?
Hili linakusaidia kujenga mtazamo wa mbele na kuepuka kufanya maamuzi ya majaribio yasiyo na msingi thabiti ndio maana watu wengi hujaribu kidogo wakiona haiwaletea faida kwa muda huo wanaacha. Anajaribu kutafuta vijana wamsaidia kupromote biashara yake mtandaoni lakini akiona haimpi matokeo anayoyataka basi anasema mitandao haisaidii wakati alitakiwa kujaribu tena na tena.
Mikakati Muhimu ya Kujenga Biashara Mtandaoni
Tengeneza Tovuti
Tovuti ni sehemu kuu ambapo kila taarifa muhimu juu ya biashara yako unayotaka mtembeleaji wa website aione basi inapaswa kuwepo.
Tumia mitandao ya kijamii kwa ufanisi
Hakikisha akaunti zako za biashara zipo active. Kama huwezi kuzisimamia mwenyewe kwa kiwango kinachoridhisha, tafuta wataalamu mbali mbali wa masoko mtandaoni wakusaidie. Sometime huwezi kuwa na lugha ya kushawishi au kwako marketing ni ngumu tafuta watu wanaojua watakusaidia kupeleka biashara mbali iwafikie watu wengi.
kujitoa kifedha na kiakili
Bila kutumia pesa huwezi kupata pesa. Kujenga jina kubwa kwa biashara yako mtandaoni kunahitaji utayari wako wa kutumia fedha kuajiri hao marketers, kulipia matangazo kwa social media na kuwa tayari kujitoa kimawazo kwa maana kuandika maudhui mtandaoni. Jitoe kuwekeza muda wako kuandaa mikakati utakayokuwa unatumia kuwasilisha kutangaza biashara yako.
Fanya maamuzi kwa haraka
Soko la kidigitali linakuhitaji mara nyingi utumie ‘Type 2 decision’ ambayo ni maamuzi ya haraka unapaswa kuyafanya kwa wakati. Ukiona mkakati wowote unafaa basi utekeleze muda huo huo usisubiri mpaka mtu fulani approve au akubali mara nyingi matokeo mazuri huja kwa kujaribu njia tofuti tofauti. Tafuta suluhisho, litathmini, na litekeleze kwa haraka maana soko lenyewe halina formula moja ya kuwafikia walengwa.
Mnaweza mkakaa management yenu mkaja na idea mbali mbali na zote zisifanye kazi ila idea ya watu wawili nje ya kikao chenu yaliyotoa huko au umeyasikia sehemu ukiyafanyia kazi unaona matokea na hii mbinu ya ndio hufanya kazi na kuleta matokeo.
Wekeza kwenye utafiti na ubunifu
Utafiki mzuri ni ule wa kuingia sokoni moja kwa moja unaweza kusom course zote za marketing na branding na ukashindwa kukuza biashara yako. Jaribu njia mbali mbali leo unakuja na hiki kesho hiki kisha sikiliza mrejesho wa soko moja kwa moja.
Uvumulivu ni Muhimu
Hakuna biashara inayofanikiwa mara moja inapoingia sokoni. Kujenga mizizi ya biashara yako mtandaoni kunahitaji muda, juhudi, na uvumilivu. Faida kubwa inaweza kuchukua miaka kuonekana, lakini uzuri wa soko la kidigitali ni kwamba linaendelea kukua kila siku hivyo ni muhimu zaidi kuwa kuvumilivu katika kipindi ambavyo utaona mambo yanaenda ndivyo sivyo.
Hitimisho
Majukwaa ya kidigitali si hiari tena bali ni lazima kila biashara inayotaka kukua na kufanikiwa iitmue kwa sababu huko ndiko soko lilipo. Usisubiri kesho chukua hatua leo Kumbuka kukua kwa biashara yako kunahitaji maamuzi utakayoyafanya leo. Anza safari yako ya kidigitali sasa.
Chukua hatua sasa na ujenge msingi imara wa mafanikio ya biashara yako kesho
0 Comments