Fahamu Jinsi ya Kuuza Bidhaa, Ujuzi Mtandaoni

Fahamu Jinsi ya Kuuza Bidhaa, Ujuzi Mtandaoni

Mtandaoni ni sehemu ambayo maajabu hutokea, mambo ambayo wengi hudhani hayawezekani huku huwa yanawezekana hasa kwako wewe unayetazamia kuuza bidhaa au ujuzi wako kupitia majukwaa ya kidigitali. 

Kabla ya yote fahamu hili, ni vigumu sana kuuza bidhaa kwa watu ambao hawakujui. Kuza jina lako kwanza watu wakufahamu ili iwe rahisi kupata wateja mtandaoni.

Watu hununua bidhaa kutoka kwa watu wanaowafahamu sasa wewe jiulize watu wanakufahamu? Siyo tu kujulikana ni kitu gani cha tofauti wanaweza kukipata kwako nao wakafaidika nacho?

Iwe ni mwanafunzi unatafuta kazi mtandaoni, iwe ni mfanya biashara unatafuta wateja mtandaoni, iwe ni mjasiriamali unataka kuuza kitabu mtandaoni, haya ni mambo muhimu inakubidi uyafahamu na kuyafanya.

Share Story yako

Hichi ni kipengele ambacho wafuasi (followers) wako hujisikia wote mko pamoja, mnapitia matatizo yale yale, wanakuchukulia kama ni wa kwao waSwahili wanasema mcheza kwao hutunzwa. 

Jenga story zako kutokana na vitu ulivyovifanya, unavyovifanya, changamoto gani ulikutana nazo na ulizitatuaje? Hapa tuelewana unapokuwa unatengeneza maudhui ya aina hii jaribu kuhusianisha story yako na changamoto ambazo watu wanazipitia kila siku.

Unaweza pia ukawa unatengeneza maudhui yanayohusu maisha ya kawaida kabisa, lengo hapa ni kujenga uaminifu ili watu wakufahamu na waendelee kukufuatilia zaidi. Watu hawanunui bidhaa au ujuzi wako wananunua jina na story zako. 

Uwepo wako mtandaoni.

Mteja akikuta duka limefungwa anaenda zake duka jingine hivyo hivyo hata katika majukwaa ya kidigitali kama huonekani kila mara. Haupost maana yake huhitaje wateja tena, maana yake umefunga biashara yako – Asiyekuwepo na lake halipo. 

Onyesha uwepo wako kwa kupost, kushiriki na creators wengine kwenye majukwaa ambayo target audience yako ipo. Uwepo wako mtandaoni ndio utakaokufanya uongeze watu wanaokufuatilia, usisahaulike mapema na kukuza jina lako pia. Utashuhudia mabo haya yakitukia kukuhusu wewe. 

  • Muone fulani huwa anafanya hiki.
  • Muone fulani atakusaidia.
  • Muone fulani huwa anazungumzia hivi vitu.

Hivi ndivyo jina lako litazidi kukua zaidi na usisahaulike kwenye masikio ya watu wanaokufuatilia. 

Uvumilivu

Kuna muda inafika kila kitu unachokifanya hakiendi, unapost lakini wapi hata likes, comment zenyewe hazionekani, hakuna maendelea yanayoonyesha matumaini yoyote siku za usoni lakini kama nilivyokwisha kusema hapo awali miujiza hutokea mtandaoni. 

Siku usiyoitegemea, saa usiyoijua, mtu ambae hujawahi kukutana nae wala ku-engage nae kwenye post zako. Mteja ambae hukuwahi kumuona tangu kuumbwa kwa ulimwengu siku hiyo anakuja inbox kwako kutaka huduma unayoitoa, kununua kitabu unachokiuza au kufanya kazi na wewe. 

Hadhira yako

Majukwaa ya kidigitali yana hadhira wanotofautiana hivyo ni vyema kujua hadhira yako ni ipi ili uweze kutengeneza maudhui yatakayowalenga moja kwa moja. Usiwe kama watu wa global climate wanaozungumzia global issues asscociated with climate. 

Ukijua hadhira yako ni Watanzania usijichoshe saana kuanza kuandika kingereza ambacho kitampa msomaje kuelewa ujumbe wako haraka fanya hivi nyooka na kiswahili mubashara ambacho hata mama mboga sokoni anaweza kukielewa.

Mtanzania anayehitaji huduma yako hataki hata kujua wewe unajua kimombo kiasi gani anachohitaji ni kutatua changamoto zake basi, liangalie hilo kwa jicho la pili.

Lakini kama hadhira yako ni wale wasiojua kiSwahili vivyo hivyo komaa na kimombo. Aidha kuna wale wa code switching ambao pia itahidi ufanye kutumia lugha zote mbili leo unapost kwa kingereza, masaa fulani kwa kiswahili. 

Kwenye kuwasilisha maudhui yako usiongee na watu wote, ongea na mtu mmoja mfano “sehemu ambayo unaweza kujifunza maarifa ya kidigitali ni Linkedin premium, je unafahamu jinsi ya kujiunga pamoja na faida zake?” hapo unaongea na mtu mmoja lakini ujumbe ni kwa wote wasioijua LinkedIn premium na faida zake. Fanya hivyo kila unapowasilisha maudhui yako itakusaidia.

Tunza malengo yako

Jiulize malengo yako ya kuwepo kwenye huo mtandao ni yapi hasa? pia jitahidi kurejea malengo yako kila mara. Kuna watu wanastruggle kidogo tu anajaribu motivation oya! Motivation zinatembea balaa. Huyoo! Kila siku unamuona anapost motivation.

Acha nikwambie ukikomaa na motivation sana utajikuta DM kweupe, hakuna kazi, hakuna fursa yoyote unayopewa japo likes kwenye post zako ni nyingi. 

Motivation hazilipi chochote labda upewe kazi ya kutangaza bidhaa fulani kwenye kurasa zako. You guy amini kile ulichonacho na onyesha watu wakujue japo mwanzo ni mgumu sana. 

Mwisho

Kuna namna nyingi za kuuza ujuzi, bidhaa mtandaoni zingine utajifunza ukiwa tayari unatumia hizi nilizoandika hapo juu.

Wazungu wanasema mistakes are the best way of learning hivyo ukipata hasara, changamoto yoyote jifunze kwayo wala usikate tamaa kwa sababu maisha lazima yaendelee.