Umuhimu wa Kutengeneza Website/Tovuti 2024
Mtu akikuangalia akaona huna website anaanza kukulianganisha na scams. Sababu biashara nyingi zilizo serious lazima utakuta zina website. Website inayobeba heshima ya biashara zao.
Website inampa mmiliki uwezo wa kufanya kile anachotaka ili kusudi ionekane yakipekee kwenye soko la kidigitali yaani akitaka website iwe na hiki, ifanye hiki, mambo gani aweke kwa namna gani, ni yeye tu.
Leo hii Akaunti zako za mitandao ikifungwa utabaki na nini au biashara yako ndio itakuwa imeshia hapo! Tafakari kisha chukua hatua.
Website ina faida kedekede kama ambavyo nimekuainishia hapa chini.
Uaminifu
Watu siku hizi hawaamini maneno kirahisi rahisi, hawaamini tu kile mtu anapost mtandaoni kwani kumekuwa na watu wengi sana huko mtandaoni wanaosema wanatoa huduma kama yako lakini ukiangalia hawana tovuti/website.
Wengi wanaamini biashara yoyote lazima iliyo serious ina website, wakikusearch halafu wakakukosa wanaanza kukutilia mashaka.
Ni mara ngapi umekuwa ukisikia au ulishawahi kuulizwa, “Je, una tovuti ninayoweza kuangalia zaidi huduma yako?” Siyo kwamba watu hawataki kununua bidhaa au kupata huduma yako! Hapana.
Wanataka kupata ushahidi na maelezo zaidi kwamba ni kweli unaweza kutimiza ahadi zako unazoahidi huko mtandaoni. Isije ukawaingiza chaka.
Ujue kila mtu anaweza kutengeneza akaunti Twitter (X), LinkedIn au Instangram lakini ni wachache wanaoweza kutengeneza website. Kuwa na website ni ishara ya kuwa wewe ni mwaminifu ndiyo maana watu huuliza una website?
Kuwa na website ni zaidi ya kuwepo mtandaoni—ni pamoja na kukujengea uaminifu wako katika enzi hizi za kidijitali. Inakuonyesha kwa wateja wako kuwa upo serios na biashara, kweli umewekeza katika biashara yako.
Bila website watu watakuwa wanakuangalia tu huko mtandaoni, utakuwa unapoteza fursa nyingi zinaenda kwa washindani wako ambao tayari wana website kali.
Tovuti/website hailali wala haichukui likizo. Ipo hewani masaa 24 ikikutangazia biashara yako. Ikiwa website imetengeneza kitaalamu, yenye mvuto, yenye maneno ya ushawishi ndani yake inaweza kukupatia faida mara dufu ndani ya muda mchache.
Website ni kwa ajili ya kuuza/kutangaza huduma yako
Shida ya makampuni mengi yanatengeneza website ili yaonekane yana website. Je hilo ndilo lengo! Website ni kwaajili ya kutangaza, kukuza biashara kisha ikupatie wateja watakaokulipa ili uwapatie huduma yako.
Usiruhusu website yako ikae tu kama haipo. Tengeneza tovuti itakayokupatia faida itakayoonyesha kazi zako, itakayotoa ushuhuda (wateja uliowahi kuwasaidia).
Imarisha uaminifu wako mtandaoni na sifa zako leo kwa njia ya website.
Tengeneza tovuti inayothibitisha unaweza kufanya unachosema, na uone jinsi inavyogeuka kuwa chombo chako cha thamani zaidi cha masoko mtandaoni.
Changamoto nyingine ambayo watu huwa wanakuja kulaumu kuwa website haisaidii. Unatengeneza website halafu huipromote yaani huitangazi kwenye mitandao ya kijamii muda huo huo unataka watu wengi waitembelee na upate wateja wengi kweli!
Website ndiyo makao makuu ya marketing ukitengeneza website isemee kwenye mitandao hivyo ndivyo unavyojitangaza na kuvutia wateja.
Mtu atayetengeneza website atafanya upate wake ionekane kwenye search engine pale mtu anaposearch kitu mtandao basi website yako ipate kupendekezwa ionekana. Pia na wewe ufanye upande wako.
Website ni utambulisho wako mkubwa mtandaoni
Website itawafanya hata watu ambao walikuwa hawakujui wakujue kwa undani kwa muda mchache. Kuliko ile mtu aanze kuscroll kwenye social media akaunti zako halafu ndo akute huo mda ulikuwa unapost mambo unayoyajua mwenyewe unafikiri.
Ataendelea kukufuatilia? Kwenye mitandao ya kijamii unaweza kupost chochote ili uchangamane na watu wengine lakini kwenye website content zinazokaa pale ni zile za muhimu tu.
Yaani ni rahisi mtu kukupa umakini zaidi hata kumfanya akupigie simu kwa majadiliano zaidi.
Jarida la leo nchini marekani –Top website statistics you should know in 2024 linasema takribani website mpya 252,000 zimekuwa zikitengenezwa kila iitwapo leo ambayo ni sawa na kusema website 10,500 zinatengenezwa kila lisaa au website 3 kila sekunde.
Hii ina maanisha ni kwa jinsi gani website zimekuwa zikifaidisha wafanya biashara wengi. Hasa wafanya biashara wanaotamani kupanua na kutangaza biashara zao mtandaoni.
Ukitaka kutengeneza website kali itakayokutangaza vizuri kwenye digitali hakikisha unaangalia na kampuni, agency, developer au designer anayeelewa fikra za wateja wako nikimaanisha saikolojia ya website development.