Yajue Malengo 3 Kabla Ya Kutengeneza Website Yako

Malengo Mubashara

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a Web Designer and Hosting @Tanzlite | Content Writer

June 19, 2024

Malengo ya kuanzisha tovuti huwa yanatofautiana kulingana na mmiliki wa tovuti hiyo. Malengo yangu na yako yanaweza yakatofautiana kulingana na mitazamo, mahitaji yetu kuwa tofauti

Kimsingi watu wengi wanaoanzisha tovuti huwa na malengo ya kupata pesa. Ukizingatia mabadiliko ya sayansi na technolojia yalivyosaidia kuunganisha watu kuwa kama kijiji, imekuwa rahisi kwa wachache kufedha hizo.

Pale watu walipo ndio pesa ilipo. Kama watu wapo mtandaoni basi pesa zipo mtandaoni.

Tuangalie malengo makuu unayotakiwa kuyangalia kabla ya kuanzisha website yako.

1) Kuuza Bidhaa

Tovuti inasaidia kuuza bidhaa uliyonayo yaweza kuwa ni nguo, vitabu, vifaa vya kielectronic, accessories n.k Hii ndio njia kuu na rahisi wanayoitumia wajasiriamali wengi wa kidigitali. 

Wajasirimali wanatumia tovuti kwa ajili ya kuuza bidhaa zao za kimwili au kidigitali. Tovuti inawasaidia kufikia watu kutoka sehemu mbalimbali. Uzuri wake ni kwamba watu wanaweza kununua bidhaa yako kwenye tovuti na kila kitu kikamalizika bila kuonana na mteja.

Kama inavyowasaidia wengine hapa Tanzania hata wewe itakusaidia kutengeneza duka lako mtandaoni na kuuza bidhaa zako. Kuna baadhi ya watanzania wamehamishia maduka yao kwenye website baada ya kuona haiwagharimu sana.

Yeye anahakikisha tu anabundle, ana simu janja basi, kazi iliyobaki ni kuhakikisha atakayenunua bidhaa anafikishiwa bidhaa yake kwa wakati. Ukiwekeza kwa namna hii utashuhudia ukipigiwa simu na wateja ambao huwajawahi kuwafikiria hata siku moja.

Mteja wako anakachokuwa anafanya ni ku-click click tu bidhaa hii hapa. Ikumbukwe: watu hununua bidhaa kutoka kwa watu wanaowajua.

Wewe unataka uanze biashara yako ya kuuza bidhaa kwa njia ya website. Jiulize, watu wanakufahamu? Watu wanaifahamu hiyo website yako, Unafahamika huko mtandaoni? Brand yako ikoje?

See also  Jinsi ya Kujiunga LinkedIn Premium Bure (na faida zake)

Lengo hili huwa ni gumu sana kulifanikisha kama hutotia nguvu na juhudi katika kutangaza bidhaa au huduma unayotamani kuiuza huko kwenye majukwaa mengine ya kidigitali.

Website itakusaidia kufanya mauzo ya bidhaa yako lakini haina uwezo mkubwa wa kuleta watu kwenye hiyo website ukiondoa injini ya utafuta (Search engine). Wewe ndiyo mwenye jukumu la kuleta watu kwenye website hiyo.

Uwezo wako wa kushawishi watu waje kwenye website yako ndio utakaokupa uwezekano wa bidhaa yako kununuliwa. Siyo rahisi lakini inawezekana ukiamua.

2. Tovuti za Washirika (Affiliate websites).

Tovuti hizi huwekwa matangazo ya bidhaa au ya huduma inayotolewa sehemu nyingine. Ulishawahi kutembelea tovuti fulani halafu ukakutana na tangazo linakutaka ubonyeze kisha linakupeleka sehemu nyingine kwenda kununua bidhaa au huduma fulani?

Naam, hizo ndio affiliate websites ninazozizungumzia. Mara nyingi matangazo haya huwekwa kwenye blogs. Mtu anapokuwa anasoma makala fulani ndani yake kuna kuwa na matangazo yanayoonyesha biashara ya mtu mwingine.

Mtu akibonyenza tangazo hilo linampeleka kwenye website inayohusu tangazo hilo. Huko ndo anaweza kufanya kile watengeneza tangazo wamekusudia. Tovuti hizi huwasaidia wenye tovuti kulipwa na kampuni ambalo wamekubali waweke tangazo lao kwenye website zao.

Ikiwa na wewe unataka utengeneza website ya aina hii hauna budi kupata kuwa mwandishi wa makala au kurasa ambazo zitakuwa zinapata watembeleaji wa kutosha.

Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kulipwa ikiwa umetengeneza tovuti yako na inapata watembeleaji wa kutosha 1. Paid per click: Mtu akibonyeza hiyo link (Tangazo) kuna asilimia mmiliki wa tovuti atakulipa. 2. Paid per contract: Mmiliki tovuti (wewe) unaingia mkataba na kampuni inayotaka iweka tangazo lake kwenye website yako.

See also  Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Kwenye affiliate websites mara nyingi huwa haina faida sana kama huna watembeleza wa kutosha wa tovuti yako. Jinsi unavyokuwa na watembeleaji wengi ndivyo utakavyoongeza nafasi ya kulipwa zaidi kulingana na makubaliano kati yako na mwenye tangazo.

Kama ulishawahi kutembelea tovuti halafu ukakuta kuna matangazo ya BETPAWA sijui BET SASA enhee! Hiyo pia ni aina ya affiliate websites.

3) Kuuza Huduma

Hapa ndipo tovuti hutumika kuongeza ufahamu zaidi juu ya kile mtu au kampuni inakiuza. Naomba tuelewane maana unaweza ukachanganya kati ya huduma na bidhaa.

Huduma inaweza kuwa utengenezaji wa wavuti, hosting services, huduma za ushauri, utoaji wa elimu kuhusu kitu fulani.  Mfano: Mimi natoa huduma ya kutengeneza website na kuhost tovuti za watu wengine. Hii siyo bidhaa ni huduma. Mwingine anaweza kusema Graphic designing na mwingine akasema Coaching.

Kwa hiyo tovuti hizi ni kwa ajili ya kuuza huduma uliyonayo. Ukienda thecitizen (Mwananchi) wanatoa huduma ya habari (magazeti), kwa mtu ambaye anataka kuwa anapata taarifa zote basi atalipia kwa mwezi au kwa mwaka ili apewe ruhusu ya kuona kila Habari inayochapishwa.

Unaweza kuamua hata wewe tuseme unatoa elimu kuhusu bima, umuhimu wake, hasara n.k kwa njia ya kozi na ukaifunga kwenye tovuti ili mtu anapotaka kozi hiyo basi aweze kuilipia. Huku ndiko kuuza huduma ninakokumaanisha.

Kwa kumalizia kasome zaidi pia umuhimu kwa kutengeneza website katika nyakati hizi za kidigitali.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also Like….

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Ukiamua kutumia digital platforms kutangaza huduma/biashara yako ili watu wengi waifahamu, wakutafute ufanye nao kazi (partners), wanunue bidhaa zako n.k inahitaji kujitoa muda wako, pesa na kuwa tayari kuendana na hali ya soko.  Kutumia majukwaa ya mtandaoni...

Mambo Ya Kuzingatia Unapotaka Kununua Hosting

Mambo Ya Kuzingatia Unapotaka Kununua Hosting

Baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye website kama loading time, performance, critical error na kushindwa kufanya baadhi ya changes hutokea kwa sababu ya hosting service uliyonunua.Wakati mwingine huwa ni teknolojia mbovu ya hosting (Outdated).Kabla ya kununua au...

You may also Like….

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Ukiamua kutumia digital platforms kutangaza huduma/biashara yako ili watu wengi waifahamu, wakutafute ufanye nao kazi (partners), wanunue bidhaa zako n.k inahitaji kujitoa muda wako, pesa na kuwa tayari kuendana na hali ya soko.  Kutumia majukwaa ya mtandaoni...

Mambo Ya Kuzingatia Unapotaka Kununua Hosting

Mambo Ya Kuzingatia Unapotaka Kununua Hosting

Baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye website kama loading time, performance, critical error na kushindwa kufanya baadhi ya changes hutokea kwa sababu ya hosting service uliyonunua.Wakati mwingine huwa ni teknolojia mbovu ya hosting (Outdated).Kabla ya kununua au...