Harakati Za Mjasiriamali Kujikomboa Zinakumbwa Na Changamoto Nyingi
Elimu yetu ningeiona ya maana sana ingekuwa inafundisha kujitegemea. Leo hii tungekuwa na viwanda vingi. Tungekuwa na ajira nyingi wahitimu, wanazengo wangejipambania wao wenyewe.
Kidogo vyuo vya ufundi (VETA) wako vizuri. 👏
Saivi elimu inaandaa vijana wazee watakaoingia ofisini kutunga sheria za tunakula vipi, kuandaa vikwazo vingi ili wajasiriamali wasiweze kuendeleza biashara zao. Inaandaa vijana wazee ili waje kuwa wakusanya kodi hodari mtaani si kuwaza ni kivipi itawasaidia wajasiriamali.
Kabla hatujapata uhuru wakoloni walichukua vijana wachache wawasomeshe ili waje wawasaidie kukusanya kodi yaani mtu akifanya kazi kwenye kiwanda chao wanamlipa mshahara kidogo bado mshahara huo huo aje alipe matiti tax, head tax, family tax hapo bado mahitaji ya familia kuna michango ya hapa na pale.
Elimu yetu bado iko huko na serikali vile vile. Hata wale wanaongia ofisini hawaelewi the hustle na namna ya kuwasaidia wajasiriamali hawa, wanaohitaji leseni, vibari ili kuendeleza mapambano yao.
Wengine wanaelewa lakini mikopo inawakaba koo.
Tuachane na hayo. Mchakato wa kupata huduma serikalini siyo rafiki kabisa, utahudhuria ofisini kwao mpaka basi mara njoo na hiki njoo na kile, lipia hiki lipia kile, mbona mtu fulani hajasaini rudi, subiri wiki mbili mtu wa.. aaprove, nenda ofisi za TANU.
Nimehangaika sana na hawa watu I know. Kwenye kutaka pesa wako chap ila kumpa huduma mapema msitahiki aah!
Kila siku upo road utafikiri mimi ni mfanyakazi wa serikali. Vitu vingine havina umuhimu lakini utasikia hatuwezi kukuhudumia bila hicho kitu.
Harakati za mjasiriamali kujikomboa zinakumbwa na changamoto nyingi hasa kwenye nchi ambayo haitambui nguvu ya mjasiriamali kwa taifa.