Mwaka 1972 mwezi wa 10 kulikuwa na safari ya wachezaji kutoka Uruguay kwenda Chile kwa ajili ya mechi waliyoisubiria kwa hamu.
Na mmoja wa wachezaji alikuwa ni Nando ambaye alimwalika pia mama yake na mdogo wake wa kike waende kumwangali the way atakavyo perform uwanjani.
Lakini safari yao iligeuka kuwa yenye majonzi na kilio. Ndege waliyokuwa wamepanda ilipata ajari njiani ikaanguka katikati ya milima mirefu kiasi kwamba mamlaka za anga za Uruguay na Chile zilijaribu kila namna kuwatafuta lakini ilishindikana.
Kwani mara tu ndege ilipoanguka watu takribani 16 walipoteza maisha pale pale akiwemo mama yake Nando pia mdogo wake naye aliaga dunia siku chache baadae.
Kitu chakusikitisha ni kwamba sehemu waliyoangukia ilikuwa ni barafu tupu hakuna miti, hakuna dalili yoyote wanaweza kupata chakula.
Ilikuwa siku ya 1, 2, 3 mara wiki, waliishiwa manju manju yote walokuwa wamebeba. Njaa mwana malevya ilianza kuwatafuna hadi ikafika muda wakawa hawana jinsi zaidi ya kuwala wenzao waliokuwa wamekufa.
Hawakuwa na jinsi yoyote ya kufanya zaidi, walianza na pilot. Wakamkata kata vipande. Wakamla.
Siku zilizidi kwenda wakifanya vivyo hivyo kwa marehemu wengine hadi pale Nando alipoona miili inayofuata ni ya mama yake na mdogo wake hapa ilimuwia vigumu sana kufanya kitendo hiko nafsi ilikataa katu katu.
Unaambiwa damu ni nzito kuliko maji alisema “Sitaki kula miili yao, sitaki hata kufanya hivyo”.
Ni bora nikafie huko mbele ya safari kuliko kukaa hapa kuwala ndugu zangu, basi kishingo upande akajifungasha machozi yakimtoka ilikuwa ngumu sana kuvumilia ila atafanya nini! alianza safari ya kupanda mlima akiwa na matumaini labda anaweza muona mtu akamsaidia lakini anakoelekea hapajui barafu imetanda kila sehemu.
Alianza safari ya kupanda mlima. Mlima ulikuwa mrefu sana kitu kilichomfanya aone kana kwamba hakuna hatua yoyote anayopiga.
Siku tatu mfululizo mguu kwa mguu anasonga. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kufika juu japo kwa kujikongoja ila kufika kwake juu hakukuleta tabasamu usoni mwake kwani safari ilikuwa ndo ka imeanza upya.
Pumzi ilianza kumwisha, nguvu zilimwisha, hawezi tena kuongea akitizama kulia, kushoto mbele ni milima mtupu.
Anasema “hiyo ndiyo siku nilijua nimekufa… Lakini hakuna namna, siwezi kurudi nilikotoka nikale miili ya mama yangu na dada yangu. Njia pekee niliyonayo ni kusonga mbele, nitakufa lakini nife huku nikijaribu kujiokoa… Nitaendelea kusonga mbele hadi pale pumzi itakapokata”
Mwanaume alijinyanyua tena na kuanza safari, siku ya 1 2 3 4 anatembea, siku ya 10 ilipofika aliona na kujisemea moyoni “Ee mungu wangu nisamehe makosa niliyokutenda naomba unipokee mikononi mwako. Ilikuwa siku yake ya roho kuagana na mwili maana kutembea kwenyewe sasa hawezi tena masikini.
Hatua za mwisho mwisho alale chini ghafla aliona kwa mbaali ka kuna mtu ana farasi. Mawazo ya kufa yalimtoka, alijawa na matumaini moyoni mwake alianza kujikongoja tena kumfuata.
Alipomkaribia tu akaanguka akazimia pale pale. Mwenye farasi alipigwa na butwaa kuona kiwili wili kinaishilizia chini akaanza kusogea kuona ni nini hicho!
Basi bwana, Nando aliokolewa namna ile baadae wenzake 14 waliobaki kw ndege wakila wenzao nao waliokolewa pia.
Mwisho.
Usikate tamaa kwa yale magumu unayokutana nayo yatapita. Endelea kusonga mbele kesho yaweza kuwa yenye furaha zaidi kuliko leo. Kesho ni fumbo.
0 Comments