Umuhimu Wa Kuwa Na Website Licha Ya Kutegemea Mitandao Ya Kijamii Kupata Wateja

Umuhimu Wa Kuwa Na Website Licha Ya Kutegemea Mitandao Ya Kijamii Kupata Wateja

Kuna swali niliwahi kuulizwa “Kama ninapata wateja na kila kitu ninachokitaka kupitia mitandao ya kijamii je, kuna umuhimu gani wa kuwa na website”

Vipi kama ungelikuwa na website, si ungekuwa unapata wateja mara mbili zaidi? 

Okay, social media siyo majukwaa yako muda wowote algorithms inaweza kubadilika, akaunti yako inaweza kufungiwa muda wowote.

Mtandaoni unaweza ukawa unapost vitu ambavyo haviendani na career yako/ business yako lakini kuna mtu akawa interested kujua zaidi “Huyu mtu anafanya nini” kama haweza kupata majibu ya direct mpaka aanze kuscroll kwenye post zako huenda na wewe wiki nzima unapost unrelated stuff maana yake hawezi kujua who you’re, what you do. Utapoteza fursa. 

Ni vigumu kuonyesha testmonials zote kwa pamoja, ni vigumu kuonyesha nini unafanya ama nini kampuni yako inafanya kwa kina ili kwamba mtu akiangalia aelewe deep nini anaweza kufaidika kutoka kwako kabla hata hajakupigia simu. 

Pili, unakuwa limited kuandika post ndefu sababu ya platform yenyewe ilivyo watu wengi hawawezi kusoma maneno mengi kiasi hicho (mfumo wa usomaji post ndefu siyo rafiki). 

Tatu, visibility yako kwa search engine ni hafifu. Watu wakisachi huduma au bidhaa kama yako huwezi kuonekana kwenye SERP (Search Engine Result Page). 

Hata kama kuna post ulijieleze au ulielezea nini kampuni yako inafanya mtu hawezi kuscroll post zote hadi aipate hiyo post. Kwanza hiyo post hajui kama ipo. 

Unataka kukusanya emails za watu ili uwe unawapatia updates kuhusu biashara yako. Social media haina tool hiyo. 

Website inatatua matatizo yote hayo na mengine mengi ambayo zijayataja. Kwa hiyo kama unategemea social media pekee fikiria mara mbili huenda ukafaidika zaidi ukiwa na website. 

Huenda kuna watu wanamaswali kuhusu wewe ila ukiwawekea testmonials pale na maelezo mengine huenda ukaongeza trust kwa watu wengi. 

Hata wote unaowaona kwa social media wenye akaunti kubwa kubwa kwa social media ukiwaangalia profile zao lazima utakuta kuna link ya either website yake au kampuni yake. 

Sidhani kama kuna mtu huko mtandaoni yuko serious na kazi yake lakini hana website.  

Stori Ya Kijana Aliyenusurika Kifo Baada ya Kukataa Kuwala Mama Na Dada Yake

Stori Ya Kijana Aliyenusurika Kifo Baada ya Kukataa Kuwala Mama Na Dada Yake

Mwaka 1972  mwezi wa 10 kulikuwa na safari ya wachezaji kutoka Uruguay kwenda Chile kwa ajili ya mechi waliyoisubiria kwa hamu. 

Na mmoja wa wachezaji alikuwa ni Nando ambaye alimwalika pia mama yake na mdogo wake wa kike waende kumwangali the way atakavyo perform uwanjani. 

Lakini safari yao iligeuka kuwa yenye majonzi na kilio. Ndege waliyokuwa wamepanda ilipata ajari njiani ikaanguka katikati ya milima mirefu kiasi kwamba mamlaka za anga za Uruguay na Chile zilijaribu kila namna kuwatafuta lakini ilishindikana. 

Kwani mara tu ndege ilipoanguka watu takribani 16 walipoteza maisha pale pale akiwemo mama yake Nando pia mdogo wake naye aliaga dunia siku chache baadae. 

Kitu chakusikitisha ni kwamba sehemu waliyoangukia ilikuwa ni barafu tupu hakuna miti, hakuna dalili yoyote wanaweza kupata chakula. 

Ilikuwa siku ya 1, 2, 3 mara wiki, waliishiwa manju manju yote walokuwa wamebeba. Njaa mwana malevya ilianza kuwatafuna hadi ikafika muda wakawa hawana jinsi zaidi ya kuwala wenzao waliokuwa wamekufa.

Hawakuwa na jinsi yoyote ya kufanya zaidi, walianza na pilot. Wakamkata kata vipande. Wakamla. 

Siku zilizidi kwenda wakifanya vivyo hivyo kwa marehemu wengine hadi pale Nando alipoona miili inayofuata ni ya mama yake na mdogo wake hapa ilimuwia vigumu sana kufanya kitendo hiko nafsi ilikataa katu katu.

Unaambiwa damu ni nzito kuliko maji alisema “Sitaki kula miili yao, sitaki hata kufanya hivyo”.

Ni bora nikafie huko mbele ya safari kuliko kukaa hapa kuwala ndugu zangu, basi kishingo upande akajifungasha machozi yakimtoka ilikuwa ngumu sana kuvumilia ila atafanya nini! alianza safari ya kupanda mlima akiwa na matumaini labda anaweza muona mtu akamsaidia lakini anakoelekea hapajui barafu imetanda kila sehemu.  

Alianza safari ya kupanda mlima. Mlima ulikuwa mrefu sana kitu kilichomfanya aone kana kwamba hakuna hatua yoyote anayopiga. 

Siku tatu mfululizo mguu kwa mguu  anasonga. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kufika juu japo kwa kujikongoja ila kufika kwake juu hakukuleta tabasamu usoni mwake kwani safari ilikuwa ndo ka imeanza upya. 

Pumzi ilianza kumwisha, nguvu zilimwisha, hawezi tena kuongea akitizama kulia, kushoto mbele ni milima mtupu. 

Anasema “hiyo ndiyo siku nilijua nimekufa… Lakini hakuna namna, siwezi kurudi nilikotoka nikale miili ya mama yangu na dada yangu. Njia pekee niliyonayo ni kusonga mbele, nitakufa lakini nife huku nikijaribu kujiokoa… Nitaendelea kusonga mbele hadi pale pumzi itakapokata” 

Mwanaume alijinyanyua tena na kuanza safari, siku ya 1 2 3 4 anatembea, siku ya 10 ilipofika aliona na kujisemea moyoni “Ee mungu wangu nisamehe makosa niliyokutenda naomba unipokee mikononi mwako. Ilikuwa siku yake ya roho kuagana na mwili maana kutembea kwenyewe sasa hawezi tena masikini. 

Hatua za mwisho mwisho alale chini ghafla aliona kwa mbaali ka kuna mtu ana farasi. Mawazo ya kufa yalimtoka, alijawa na matumaini moyoni mwake alianza kujikongoja tena kumfuata. 

Alipomkaribia tu akaanguka akazimia pale pale.  Mwenye farasi alipigwa na butwaa kuona kiwili wili kinaishilizia chini akaanza kusogea kuona ni nini hicho!  

Basi bwana, Nando aliokolewa namna ile baadae wenzake 14 waliobaki kw ndege wakila wenzao nao waliokolewa pia. 

Mwisho. 

Usikate tamaa kwa yale magumu unayokutana nayo yatapita. Endelea kusonga mbele kesho yaweza kuwa yenye furaha zaidi kuliko leo. Kesho ni fumbo.

Harakati Za Mjasiriamali Kujikomboa Zinakumbwa Na Changamoto Nyingi

Harakati Za Mjasiriamali Kujikomboa Zinakumbwa Na Changamoto Nyingi

Elimu yetu ningeiona ya maana sana ingekuwa inafundisha kujitegemea. Leo hii tungekuwa na viwanda vingi. Tungekuwa na ajira nyingi wahitimu, wanazengo wangejipambania wao wenyewe.

Kidogo vyuo vya ufundi (VETA) wako vizuri. 👏

Saivi elimu inaandaa vijana wazee watakaoingia ofisini kutunga sheria za tunakula vipi, kuandaa vikwazo vingi ili wajasiriamali wasiweze kuendeleza biashara zao. Inaandaa vijana wazee ili waje kuwa wakusanya kodi hodari mtaani si kuwaza ni kivipi itawasaidia wajasiriamali.

Kabla hatujapata uhuru wakoloni walichukua vijana wachache wawasomeshe ili waje wawasaidie kukusanya kodi yaani mtu akifanya kazi kwenye kiwanda chao wanamlipa mshahara kidogo bado mshahara huo huo aje alipe matiti tax, head tax, family tax hapo bado mahitaji ya familia kuna michango ya hapa na pale.

Elimu yetu bado iko huko na serikali vile vile. Hata wale wanaongia ofisini hawaelewi the hustle na namna ya kuwasaidia wajasiriamali hawa, wanaohitaji leseni, vibari ili kuendeleza mapambano yao.

Wengine wanaelewa lakini mikopo inawakaba koo.

Tuachane na hayo. Mchakato wa kupata huduma serikalini siyo rafiki kabisa, utahudhuria ofisini kwao mpaka basi mara njoo na hiki njoo na kile, lipia hiki lipia kile, mbona mtu fulani hajasaini rudi, subiri wiki mbili mtu wa.. aaprove, nenda ofisi za TANU.

Nimehangaika sana na hawa watu I know. Kwenye kutaka pesa wako chap ila kumpa huduma mapema msitahiki aah!

Kila siku upo road utafikiri mimi ni mfanyakazi wa serikali. Vitu vingine havina umuhimu lakini utasikia hatuwezi kukuhudumia bila hicho kitu.

Harakati za mjasiriamali kujikomboa zinakumbwa na changamoto nyingi hasa kwenye nchi ambayo haitambui nguvu ya mjasiriamali kwa taifa.

Kujifunza Web Design Ni Rahisi

Kujifunza Web Design Ni Rahisi

Kujifunza web design na ukaimaster vizuri ni rahisi sana ikiwa tu utapata mtu anayejua na amekuwa akifanya hiko kitu miaka mingi kuliko kukomaa mwenyewe.

Utapita njia fupi ambayo ulitakiwa kujifunza miaka mitatu wewe ukajifunza ndani ya mwezi mmoja au miwili. Hapo unapata muda mwingi wa kutafuta wateja, kufanya kazi za kampuni zinazohusu website.

Pia utaokoa fedha nyingi. Mimi kipindi najifunza web design huko YouTube na kwingine hasa mwaka 2023 pesa ya bundle kwa siku ilikuwa 3k kwa 6k na hapo huna client na unajibana ukipiga kwa mwezi ni 60k+

Vingine nimekuja kuvielewa 2024. Hapa katikati 2023- 2024 kuna pesa nyingi sana imepotea lakini kidogo ukipata wateja ndio mambo yanakaa mkao.

Maisha ya kujifunza mwenyewe ni stressful na pengine usijue mambo kwa kina ila ukipata mtu wa kukufundisha na ukawa serious ni simple sana. Haichukui muda.

Yajue Malengo 3 Kabla Ya Kutengeneza Website Yako

Yajue Malengo 3 Kabla Ya Kutengeneza Website Yako

Malengo ya kuanzisha tovuti huwa yanatofautiana kulingana na mmiliki wa tovuti hiyo. Malengo yangu na yako yanaweza yakatofautiana kulingana na mitazamo, mahitaji yetu kuwa tofauti

Kimsingi watu wengi wanaoanzisha tovuti huwa na malengo ya kupata pesa. Ukizingatia mabadiliko ya sayansi na technolojia yalivyosaidia kuunganisha watu kuwa kama kijiji, imekuwa rahisi kwa wachache kufedha hizo.

Pale watu walipo ndio pesa ilipo. Kama watu wapo mtandaoni basi pesa zipo mtandaoni.

Tuangalie malengo makuu unayotakiwa kuyangalia kabla ya kuanzisha website yako.

1) Kuuza Bidhaa

Tovuti inasaidia kuuza bidhaa uliyonayo yaweza kuwa ni nguo, vitabu, vifaa vya kielectronic, accessories n.k Hii ndio njia kuu na rahisi wanayoitumia wajasiriamali wengi wa kidigitali. 

Wajasirimali wanatumia tovuti kwa ajili ya kuuza bidhaa zao za kimwili au kidigitali. Tovuti inawasaidia kufikia watu kutoka sehemu mbalimbali. Uzuri wake ni kwamba watu wanaweza kununua bidhaa yako kwenye tovuti na kila kitu kikamalizika bila kuonana na mteja.

Kama inavyowasaidia wengine hapa Tanzania hata wewe itakusaidia kutengeneza duka lako mtandaoni na kuuza bidhaa zako. Kuna baadhi ya watanzania wamehamishia maduka yao kwenye website baada ya kuona haiwagharimu sana.

Yeye anahakikisha tu anabundle, ana simu janja basi, kazi iliyobaki ni kuhakikisha atakayenunua bidhaa anafikishiwa bidhaa yake kwa wakati. Ukiwekeza kwa namna hii utashuhudia ukipigiwa simu na wateja ambao huwajawahi kuwafikiria hata siku moja.

Mteja wako anakachokuwa anafanya ni ku-click click tu bidhaa hii hapa. Ikumbukwe: watu hununua bidhaa kutoka kwa watu wanaowajua.

Wewe unataka uanze biashara yako ya kuuza bidhaa kwa njia ya website. Jiulize, watu wanakufahamu? Watu wanaifahamu hiyo website yako, Unafahamika huko mtandaoni? Brand yako ikoje?

Lengo hili huwa ni gumu sana kulifanikisha kama hutotia nguvu na juhudi katika kutangaza bidhaa au huduma unayotamani kuiuza huko kwenye majukwaa mengine ya kidigitali.

Website itakusaidia kufanya mauzo ya bidhaa yako lakini haina uwezo mkubwa wa kuleta watu kwenye hiyo website ukiondoa injini ya utafuta (Search engine). Wewe ndiyo mwenye jukumu la kuleta watu kwenye website hiyo.

Uwezo wako wa kushawishi watu waje kwenye website yako ndio utakaokupa uwezekano wa bidhaa yako kununuliwa. Siyo rahisi lakini inawezekana ukiamua.

2. Tovuti za Washirika (Affiliate websites).

Tovuti hizi huwekwa matangazo ya bidhaa au ya huduma inayotolewa sehemu nyingine. Ulishawahi kutembelea tovuti fulani halafu ukakutana na tangazo linakutaka ubonyeze kisha linakupeleka sehemu nyingine kwenda kununua bidhaa au huduma fulani?

Naam, hizo ndio affiliate websites ninazozizungumzia. Mara nyingi matangazo haya huwekwa kwenye blogs. Mtu anapokuwa anasoma makala fulani ndani yake kuna kuwa na matangazo yanayoonyesha biashara ya mtu mwingine.

Mtu akibonyenza tangazo hilo linampeleka kwenye website inayohusu tangazo hilo. Huko ndo anaweza kufanya kile watengeneza tangazo wamekusudia. Tovuti hizi huwasaidia wenye tovuti kulipwa na kampuni ambalo wamekubali waweke tangazo lao kwenye website zao.

Ikiwa na wewe unataka utengeneza website ya aina hii hauna budi kupata kuwa mwandishi wa makala au kurasa ambazo zitakuwa zinapata watembeleaji wa kutosha.

Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kulipwa ikiwa umetengeneza tovuti yako na inapata watembeleaji wa kutosha 1. Paid per click: Mtu akibonyeza hiyo link (Tangazo) kuna asilimia mmiliki wa tovuti atakulipa. 2. Paid per contract: Mmiliki tovuti (wewe) unaingia mkataba na kampuni inayotaka iweka tangazo lake kwenye website yako.

Kwenye affiliate websites mara nyingi huwa haina faida sana kama huna watembeleza wa kutosha wa tovuti yako. Jinsi unavyokuwa na watembeleaji wengi ndivyo utakavyoongeza nafasi ya kulipwa zaidi kulingana na makubaliano kati yako na mwenye tangazo.

Kama ulishawahi kutembelea tovuti halafu ukakuta kuna matangazo ya BETPAWA sijui BET SASA enhee! Hiyo pia ni aina ya affiliate websites.

3) Kuuza Huduma

Hapa ndipo tovuti hutumika kuongeza ufahamu zaidi juu ya kile mtu au kampuni inakiuza. Naomba tuelewane maana unaweza ukachanganya kati ya huduma na bidhaa.

Huduma inaweza kuwa utengenezaji wa wavuti, hosting services, huduma za ushauri, utoaji wa elimu kuhusu kitu fulani.  Mfano: Mimi natoa huduma ya kutengeneza website na kuhost tovuti za watu wengine. Hii siyo bidhaa ni huduma. Mwingine anaweza kusema Graphic designing na mwingine akasema Coaching.

Kwa hiyo tovuti hizi ni kwa ajili ya kuuza huduma uliyonayo. Ukienda thecitizen (Mwananchi) wanatoa huduma ya habari (magazeti), kwa mtu ambaye anataka kuwa anapata taarifa zote basi atalipia kwa mwezi au kwa mwaka ili apewe ruhusu ya kuona kila Habari inayochapishwa.

Unaweza kuamua hata wewe tuseme unatoa elimu kuhusu bima, umuhimu wake, hasara n.k kwa njia ya kozi na ukaifunga kwenye tovuti ili mtu anapotaka kozi hiyo basi aweze kuilipia. Huku ndiko kuuza huduma ninakokumaanisha.

Kwa kumalizia kasome zaidi pia umuhimu kwa kutengeneza website katika nyakati hizi za kidigitali.