Mtandaoni ni sehemu ambayo maajabu hutokea, yalinitokea mimi mwishoni mwa mwaka 2022 nami nikasadiki kuwa mambo ambayo wengi hudhani hayawezekani huku mtandaoni yanawezekana hasa kwa yule anayetazamia kuuza bidhaa au ujuzi wake kupitia majukwaa ya kidigitali.
Mwishoni mwa maka 2022 nilipata deal ya kutengeneza website ya HR mmoja ambaye alinitafuta kutoka LinkedIn baadae nilimaliza website yake Better Career. Lakini kabla ya yote naomba ufahamu hili, ni vigumu sana kuuza bidhaa kwa watu ambao hawakujui. Ukitaka kuanza hizi mbanga jitahidi kukuza jina lako kwanza watu wakufahamu ndo uanze harakati za kutafuta wateja mtandaoni au nenda navyo vyote.
Kama wasemavyo, watu hununua bidhaa kutoka kwa watu wanaowafahamu. Sasa wewe jiulize watu wanakufahamu? Siyo tu kujulikana ni kitu gani cha tofauti wanaweza kukipata kwako nao wakafaidika nacho?
Katika ulingo wa watafutaji mtandaoni kitu pekee unaweza kutoboa ni kuonyesha upekee katika kile unachokifanya. Mwadishi mmoja aliwahi kusema “Ogopa sana kuwa mtu wa kawaida, kuwa mtu wa tofauti”.
Iwe ni mwanafunzi unatafuta kazi mtandaoni, iwe ni mfanya biashara unatafuta wateja mtandaoni, iwe ni mjasiriamali unataka kuuza vitu mtandaoni, haya ni mambo muhimu inakubidi uyafahamu na kuyafanya.
Share Story yako
Hichi ni kipengele ambacho wafuasi (followers) wako hujisikia wote mko pamoja, mnapitia matatizo yale yale, wanakuchukulia kama ni wa kwao waSwahili wanasema mcheza kwao hutunzwa. Binafsi 2022, 2023 nimekaa LinkedIn almost mwaka mzima sijapata mteja yeyote mpaka niliona kuwa watu wakipost kuwa wanapata wateja kutoka LinkedIn ni uongo tu. Inakuwaje wao wanapata halafu mimi sipati? Nilifurukuta mpaka basi.
Asante mungu mwisho mwa mwaka 2023 ndio niliona maajabu yakishuka kutoka LinkedIn mara paa! mtu from nowhere ananitafuta WhatsApp. Walio wateja kweli kweli huwa hawanaga mbwe mbwe nyingi, akiona unachokifanya anakunyokea live DM nina kazi hii je unaweza kuifanya?Hii ni baada ya kuandika nakala kadhaa juu kile ninchokifanya.
Hivyo, Jenga hoja/story zako kutokana na vitu ulivyovifanya, unavyovifanya, changamoto gani ulikutana nazo na ulizitatuaje? Hapa tuelewana unapokuwa unatengeneza maudhui ya aina hii jaribu kuhusianisha story yako na changamoto ambazo watu wanazipitia kila siku.
Unaweza pia ukawa unatengeneza maudhui yanayohusu maisha ya kawaida kabisa, lengo hapa ni kujenga uaminifu ili watu wakufahamu na waendelee kukufuatilia zaidi. Watu hawanunui bidhaa au ujuzi wako wananunua jina na story zako.
Uwepo wako mtandaoni.
Tusema, mteja akikuta duka limefungwa ataenda zake duka jingine. Vivyo hivyo hata katika majukwaa ya kidigitali kama huonekani kila mara. Haupost mara kwa mara maana yake maana yake umefunga biashara yako – Asiyekuwepo na lake halipo.
Onyesha uwepo wako mtandaoni kwa kupost, kushiriki na creators wengine kwenye majukwaa ambayo target audience yako ipo. Uwepo wako mtandaoni ndio utakaokufanya uongeze watu wanaokufuatilia, usisahaulike mapema na kukuza jina lako pia. Utashuhudia mambo haya yakitukia kukuhusu wewe.
- Muone fulani huwa anafanya hiki.
- Muone fulani atakusaidia.
- Muone fulani huwa anazungumzia hivi vitu.
Hivi ndivyo jina lako litazidi kukua zaidi na usisahaulike kwenye masikio ya watu wanaokufuatilia.
Uvumilivu
Kuna muda inafika kila kitu unachokifanya hakiendi, unapost lakini wapi hata likes, comment zenyewe hazionekani. Hakuna maendeleo yanayoonyesha matumaini yoyote siku za usoni lakini kama nilivyokwisha kusema hapo awali miujiza hutokea mtandaoni.
Siku usiyoitegemea, saa usiyoijua, mtu ambae hujawahi kukutana nae wala ku-engage nae kwenye post zako. Mteja ambae hukuwahi kumuona tangu kuumbwa kwa ulimwengu siku hiyo anakuja inbox kwako kutaka huduma unayoitoa, kununua kitabu unachokiuza au kufanya kazi na wewe.
Game ya mtandaoni ni kuwa mvumilivu. There is no short cut. Watu watakupa kazi, watanunua huduma yako kutokana na uwekezaji ulioweka miezi au miaka iliyopita. Kitu ambacho siku zote huwa nasema unaweza usione matokea yake leo ila baada ya miezi au miaka miwili ijayo maajabu yakaanza kukutiririkia. Ni ngumu hivyo inabidi uwe mgumu kufanikiwa.
Usione watu wanafanikiwa mtandaoni wanahaso balaa sema tu huwezi kuona wanavyohangaika behind the scene. Watu hawali ili mkono uende kinywani. Wanajaribu mbinu mbali mbali pengine kulipia course ili kujifunza zaidi hii yote ni kwa sababu wameamua kupambana mpaka mwisho.
Hadhira yako
Majukwaa ya kidigitali yana hadhira wanotofautiana hivyo ni vyema kujua hadhira yako ni ipi ili uweze kutengeneza maudhui yatakayowalenga moja kwa moja. Usiwe kama watu wa global climate wanaozungumzia global issues asscociated with climate.
Ukijua hadhira yako ni Watanzania usijichoshe saana kuanza kuandika kingereza ambacho kitampa msomaje ugumu wa kuelewa ujumbe wako kwa haraka fanya hivi nyooka na kiswahili mubashara ambacho hata mama mboga sokoni anaweza kukielewa.
Mtanzania anayehitaji huduma yako hataki hata kujua wewe unajua kimombo kiasi gani anachohitaji ni kutatua changamoto zake basi, liangalie hilo kwa jicho la pili.
Lakini kama hadhira yako ni wale wasiojua kiSwahili vivyo hivyo komaa na kimombo. Aidha kuna wale wa code switching ambao pia hutumia lugha zote mbili leo unapost kwa kingereza, masaa fulani kwa kiswahili. Ni vizuri pia.
Kwenye kuwasilisha maudhui yako usiongee na watu wote, ongea na mtu mmoja mfano “sehemu ambayo unaweza kujifunza maarifa ya kidigitali ni Linkedin premium, je unafahamu jinsi ya kujiunga pamoja na faida zake?” hapo unaongea na mtu mmoja lakini ujumbe ni kwa wote wasioijua LinkedIn premium na faida zake. Fanya hivyo kila unapowasilisha maudhui yako itakusaidia.
Jenga hoja zako kana kwamba unaongea na mtu mmoja. Hii itakusaidia sana katika kufikisha ujumbe wako kwa haraka na kwa wepesi zaidi.
Tunza malengo yako
Jiulize malengo yako ya kuwepo kwenye huo mtandao ni yapi hasa? pia jitahidi kurejea malengo yako kila mara. Kuna watu wanastruggle kidogo tu anaona mambo hayaendi, Acha agonge motivation oya! Motivation zinatembea balaa. Huyoo! Kila siku unamuona anapost motivation siyo mbaya lakini jiulize lengo lako ndio hilo au umetoka nje ya mstari.
Acha nikwambie ukikomaa na motivation sana utajikuta DM kweupe, hakuna kazi, hakuna fursa yoyote unayopewa japo likes kwenye post zako ni buku.
Motivation hazilipi chochote labda upewe kazi ya kutangaza bidhaa fulani kwenye kurasa zako. You guy amini kile ulichonacho na onyesha watu wakujue japo mwanzo ni mgumu sana.
Tatizo ni moja sisi tunataka matokeo ya haraka kwa muda mfupi yaani ni sawa na mtu anayebeti kwa buku akitegemea atapata milioni ikifika jioni. Utasubiri sana kila odd unayoweka inagonga mwamba.
Komaa na niche yako uliyochagua hata kama kila mmoja ataenda kinyume na wewe. Hata kama wengine walishindwa we komaa wewe siyo wao kila mtu ana njia yake kikubwa hutoki nje ya lengo lako.
Mwisho
Kuna namna nyingi za kuuza ujuzi, bidhaa mtandaoni zingine utajifunza ukiwa tayari unatumia hizi nilizoandika hapo juu.
Wazungu wanasema mistakes are the best way of learning hivyo ukipata hasara, changamoto yoyote jifunze kwayo wala usikate tamaa kwa sababu maisha lazima yaendelee.
0 Comments