Mambo Ya Kuzingatia Unapotaka Kununua Hosting

Web hosting

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a Web Designer and Hosting @Tanzlite | Content Writer

December 30, 2024

Baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye website kama loading time, performance, critical error na kushindwa kufanya baadhi ya changes hutokea kwa sababu ya hosting service uliyonunua.

Wakati mwingine huwa ni teknolojia mbovu ya hosting (Outdated).

Kabla ya kununua au kutafuta mchawi ni nani ni vizuri kuangalia mambo yafuatayo unapochagua web hosting provider wa website yako.


1. Disc Space.


Je, space unayoitaka inatosha kuhost mafile yako. Je, 1GB inatosha ku-upload hizo picha? inatosha Ku-upload hizo document? inatosha kushare mafaili yenye MB 30 kila siku?

Ikiwa Space itakuwa ndogo kuliko vitu unavyo-upload tegemea baadae kukutana na critical error, unable to upload, poor performance, internal sever error n.k


2. Email Account.


Unataka kutengeneza official emails ngapi, matumizi yake yatakuwaje.  Emails zinakula space sana so ikiwa hizo email utakazotengeneza zitakuwa zinapokea na kutuma mafaili yenye MB nyingi.

Ni vyema pia kuliangalia hilo japo huwa halina shida saana maana email zingine unaweza kuzifuta hasa ukiona siyo za muhimu kuendelea kuwepo kwenye database.


3. Security.


Security hasa upande wa back-end ikoje. SSL Installation. Backup inafanyika mara ngapi. Suala la site kwenda down huwa linatokea usisahau hilo either upande wa hosting ama shida yoyote inaweza kutokea hapa katikati hivyo ni vyema kujua back-up inafanyikaje. Itakuwa haipendezi website umeitengeneza halafu ghafula website ikaenda na kila kitu kikapotea.


4. Technical Support.


Je, ikitokea kuna shida ni kwa haraka gani utapata msaada? Utapata technical support kwa njia gani?

Ni vizuri ukajiulize hayo maswali na ukafanye maamuzi mapema usije ukaingia gharama isiyo lazima.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also Like….

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Ukiamua kutumia digital platforms kutangaza huduma/biashara yako ili watu wengi waifahamu, wakutafute ufanye nao kazi (partners), wanunue bidhaa zako n.k inahitaji kujitoa muda wako, pesa na kuwa tayari kuendana na hali ya soko.  Kutumia majukwaa ya mtandaoni...

Kujifunza Web Design Ni Rahisi

Kujifunza Web Design Ni Rahisi

Kujifunza web design na ukaimaster vizuri ni rahisi sana ikiwa tu utapata mtu anayejua na amekuwa akifanya hiko kitu miaka mingi kuliko kukomaa mwenyewe.Utapita njia fupi ambayo ulitakiwa kujifunza miaka mitatu wewe ukajifunza ndani ya mwezi mmoja au miwili. Hapo...

You may also Like….

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Jinsi Majukwaa ya Kidigitali Yatakavyokusaidia Kukuza Biashara Yako

Ukiamua kutumia digital platforms kutangaza huduma/biashara yako ili watu wengi waifahamu, wakutafute ufanye nao kazi (partners), wanunue bidhaa zako n.k inahitaji kujitoa muda wako, pesa na kuwa tayari kuendana na hali ya soko.  Kutumia majukwaa ya mtandaoni...