Jinsi ya Kuuza Bidhaa, Ujuzi Kupitia WhatsApp Business

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a young Website Developer and Designer. He Creates Clean, Responsive, and Converting Websites for Business Growth.

December 22, 2023

Siku moja nilikuwa nimekaa zangu ghetto mida ya saa kumi na mbili jioni nasoma Hekaya za Abunuwasi, ghafla ujumbe ukatumwa kupitia whatsApp kutoka kwa rafiki yangu akisema nimsaidie kutangaza hard disc drive aliyokuwa anauza.

Bila hiana kesho yake nikaipost kwenye status yangu, baada ya muda mfupi  habari njema zikaanza kuonekana kwenye whatsApp chat na hatimae hard disc hiyo iliweza kununuliwa. 

Tangu siku hiyo, Fikra zangu kuhusu WhatsApp zilibadilika kabisa nikajisemea moyoni “Kumbe WhatsApp inaweza kuwa iko vizuri zaidi kuliko Twitter na Instagram!” Kwamba kupitia status unaweza kuuza kitu chochote na watu wakanunua. 

Unapataje wateja?

Simple, mteja ni yeyote yule anayeweza kuona status zako. Anaweza asiwe mteja wako moja kwa moja lakini akawa na marafiki zake wanaohitaji bidhaa unayouza, kupitia yeye utapata wateja ambao wao pia wana marafiki zao wengine hivyo utajikuta umepanua biashara yako.

Utakuwa unatafutwa na watu ambao hujawahi hata kuonana nao wala kuongea nao hapo mwanzo. Jambo siyo rahisi kivile mwanzo siku zote ni mgumu lakini mdogo mdogo ukikomaa utaona matokeo yake.  

Haikugharimu chochote kupost vitu unavyouza kwenye WhatsApp status yako. Vijana wengine wanaogopa kujulikana kuwa wanafanya biashara fulani ndo mana huwa hawapost kazi zao. 

Kama ni mjasiriamali mkubwa unaweza kujifunza zaidi jinsi ya kutumia WhatsApp business kuuza na kutangaza biashara yako.

Unamwogopa nani, unahofia nini au  kazi unayoifanya ni haramu? WhatsApp ni fursa moja nzuri ambayo wachache wanaojua kuitumia vizuri wanafaidika sana.  

WhatsApp Channel na WhatsApp Group.

Kabla ya kuongezwa kwa WhatsApp channel feature wengi walikuwa wanatumia whatsapp group kuendesha shughuli zao mbali mbali ikiwemo uelemishaji, seminas, kupashana habari pamoja na kufanya biashara zao huko. 

Lakini kila kukicha mambo mapya yanaibuliwa leo hii tuna WhatsApp Channel inayokupa fursa ya kuwafikia mamilioni ya watu wanaokadiliwa kuwa ni 2.78billion na wanazidi kuongezeka kila siku. 

See also  Jinsi ya Kujiunga LinkedIn Premium Bure (na faida zake)

Kuna uwezekano mkubwa wa channel utakayotengeneza kuonekana kwa watu wengi wanaotumia WhatsApp kwa sababu by default iko public, yeyote anaweza kufollow channel hiyo. Nadhani ulishawahi kuziona kwenye whatsapp yako kama ambavyo zinaonekana kwangu hapa. 

Jinsi ya kutengeneza WhatsApp Channel

Kutengeneza WhatsApp chanell ni rahisi kabisa fungua application yako ya WhatsApp, nenda kwenye updates 

  • Bonyeza alama ya kujumuisha 
  • Create channel 
  • Click continue 
  • Upload profile picture, Channel name na description.
  • Click Continue 

Hapo utakuwa tayari umeshatengeneza WhatsApp channel kinachofuata ni wewe kuendeleza channel yako.

Jinsi ya kutafuta fursa za kazi kupitia WhatsApp. 

Kwa anayetafuta kazi au bado ni mwanafunzi, whatsapp ni sehemu nzuri ya kutangaza na kuonyesha uwezo ulionao juu ya kazi fulani.

Hapa unaweza ukawa unapost mambo ya kawaida kuhusu vitu unavyofanya, unavyovifahamu mfano graphics design, web development, afya, utalii, cryptocurrency n.k.  

Fursa haziji hivi hivi  ukiwa umelala nakumbuka siku za nyuma nilikuwa nashiriki kwenye mijadala kwenye magroup ya watu wengine huko nilijitahidi kutoa mchango wangu kulingana na uelewa wangu kuhusu mada walizokuwa wanazungumzia na uhalisia wa mambo yalivyo, pale walipoenenda tofauti niliwaambia. 

Aisee kama unajua unajua tu ilikuwa saa nne usiku kiongozi wa hilo group akanitumia ujumbe kama unavyosomeka hapo chini.

Mtu akianza kukutafuta kwa njia kama hizi jua kuna kazi umefanya, hizi ndiyo connection. Unatangaza na kukuza jina kwa style kama hii. 

Ninachotaka kusema ni kwamba fursa za kazi zinaweza kupatikana sehemu yoyote ile siyo lazima uende kuomba kazi maofisini hata kupitia whatsApp unaweza kufanikisha hili.

Hao hao watu unaobonga nao kila siku wanaweza wakakurecommend sehemu kutokana na vitu ambavyo huwa unashare nao. 

Watu hatufanani leo hii mko wote sawa kesho mwenzako manager wewe mtafuta ajira kwa hiyo siku moja historia inaweza kukubeba manager kaona kuna kazi uwezekano wa kukujulisha au kukuita ni mkubwa kwa sababu alishawahi kuona mambo unayofanya na ni yanauhusiano na kazi iliyopo.

See also  Fahamu Jinsi ya Kuuza Bidhaa, Ujuzi Mtandaoni

Sasa vipi kama ungekuwa unaongea pointless ukiwa na wenzako je, unaweza kweli ukaitwa kwa style hii? Hapana huwezi. 

Kama ni kijana jitahidi kuheshimu wenzako kwenye magroup wanapojadili mada zao hata kama wote mko level moja.

Chukulia hiyo ndiyo fursa ya kujitangaza na kuonyesha umahili wako huwezi kujua huko mbeleni mambo yanaweza kuwaje. Kuwa serious hiyo ni fursa itumie vizuri. 

Kupitia WhatsApp status.

Vijana hasa wale wanaosoma huwa hawataki kuonyesha kile wanachokijua. Utakuta kwenye status ameweka memes mwanzo mwisho, picha zao mwanzo mwisho, vichekesho mwanzo mwisho yaani hakuna hata kiashiria kinachoonyesha ujuzi wao. 

Siyo mbaya lakini kitu cha kujiuliza ni kuwa unaacha nini kwenye vichwa vya waangaliaji wa status zako. Mtu akiangalia status zako mbili tatu anaweza kujua akili yako ikoje na una mawazo yapi.

Kama kweli unataka kutafuta kazi kupitia WhatsApp jaribu angalau kuwa open kwenye status zako sema ni nini unajua, unafanyaje na unaweza kumsaidia nani.

Unaweza usione matokea kwa muda huo lakini baada ya muda utaanza kutafutwa. Nimeshasema usimdharau mtu kwa kuangalia hadhi aliyonayo leo. 

Yote kwa yote mchukulie mtu anaeangalia status zako kama mwajiri wako wa baadae. Jiamini na careers yako hata kama hutakuja kuwa huyo uliye leo kuna kitu lazima utajifunza.  

Mwisho.

Fursa nyingi tunazo mikononi mwetu, pesa tumezishikilia lakini bado tunahangaika kutumia njia ngumu katika kusaka tonge. WhatsApp ipo kwa ajili yako wewe mwenye maono ya mbali. Siku zote kazi zipo je, unazitafutaje, wateja wapo kila siku shida unawatafutaje? Maamuzi yako leo ndiyo matokeo ya kesho.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also Like….

Jinsi ya Kujiunga LinkedIn Premium Bure (na faida zake)

Jinsi ya Kujiunga LinkedIn Premium Bure (na faida zake)

Je, ulishawahi kujaribu kujiunga linkedin premium ukashindwa? Ulishindwa kwa sababu ni ya kulipia? Linkedin premium ina faida gani? Au hujawahi kabisa kufikiria kuhusu Linkedin premium? Leo nimekusogezea hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga Linkedin premium bure na faida...