Baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye website kama loading time, performance, critical error na kushindwa kufanya baadhi ya changes hutokea kwa sababu ya hosting service uliyonunua.
Wakati mwingine huwa ni teknolojia mbovu ya hosting (Outdated).
Kabla ya kununua au kutafuta mchawi ni nani ni vizuri kuangalia mambo yafuatayo unapochagua web hosting provider wa website yako.
1. Disc Space.
Je, space unayoitaka inatosha kuhost mafile yako. Je, 1GB inatosha ku-upload hizo picha? inatosha Ku-upload hizo document? inatosha kushare mafaili yenye MB 30 kila siku?
Ikiwa Space itakuwa ndogo kuliko vitu unavyo-upload tegemea baadae kukutana na critical error, unable to upload, poor performance, internal sever error n.k
2. Email Account.
Unataka kutengeneza official emails ngapi, matumizi yake yatakuwaje. Emails zinakula space sana so ikiwa hizo email utakazotengeneza zitakuwa zinapokea na kutuma mafaili yenye MB nyingi.
Ni vyema pia kuliangalia hilo japo huwa halina shida saana maana email zingine unaweza kuzifuta hasa ukiona siyo za muhimu kuendelea kuwepo kwenye database.
3. Security.
Security hasa upande wa back-end ikoje. SSL Installation. Backup inafanyika mara ngapi. Suala la site kwenda down huwa linatokea usisahau hilo either upande wa hosting ama shida yoyote inaweza kutokea hapa katikati hivyo ni vyema kujua back-up inafanyikaje. Itakuwa haipendezi website umeitengeneza halafu ghafula website ikaenda na kila kitu kikapotea.
4. Technical Support.
Je, ikitokea kuna shida ni kwa haraka gani utapata msaada? Utapata technical support kwa njia gani?
Ni vizuri ukajiulize hayo maswali na ukafanye maamuzi mapema usije ukaingia gharama isiyo lazima.
Kuna swali niliwahi kuulizwa “Kama ninapata wateja na kila kitu ninachokitaka kupitia mitandao ya kijamii je, kuna umuhimu gani wa kuwa na website”
Vipi kama ungelikuwa na website, si ungekuwa unapata wateja mara mbili zaidi?
Okay, social media siyo majukwaa yako muda wowote algorithms inaweza kubadilika, akaunti yako inaweza kufungiwa muda wowote.
Mtandaoni unaweza ukawa unapost vitu ambavyo haviendani na career yako/ business yako lakini kuna mtu akawa interested kujua zaidi “Huyu mtu anafanya nini” kama haweza kupata majibu ya direct mpaka aanze kuscroll kwenye post zako huenda na wewe wiki nzima unapost unrelated stuff maana yake hawezi kujua who you’re, what you do. Utapoteza fursa.
Ni vigumu kuonyesha testmonials zote kwa pamoja, ni vigumu kuonyesha nini unafanya ama nini kampuni yako inafanya kwa kina ili kwamba mtu akiangalia aelewe deep nini anaweza kufaidika kutoka kwako kabla hata hajakupigia simu.
Pili, unakuwa limited kuandika post ndefu sababu ya platform yenyewe ilivyo watu wengi hawawezi kusoma maneno mengi kiasi hicho (mfumo wa usomaji post ndefu siyo rafiki).
Tatu, visibility yako kwa search engine ni hafifu. Watu wakisachi huduma au bidhaa kama yako huwezi kuonekana kwenye SERP (Search Engine Result Page).
Hata kama kuna post ulijieleze au ulielezea nini kampuni yako inafanya mtu hawezi kuscroll post zote hadi aipate hiyo post. Kwanza hiyo post hajui kama ipo.
Unataka kukusanya emails za watu ili uwe unawapatia updates kuhusu biashara yako. Social media haina tool hiyo.
Website inatatua matatizo yote hayo na mengine mengi ambayo zijayataja. Kwa hiyo kama unategemea social media pekee fikiria mara mbili huenda ukafaidika zaidi ukiwa na website.
Huenda kuna watu wanamaswali kuhusu wewe ila ukiwawekea testmonials pale na maelezo mengine huenda ukaongeza trust kwa watu wengi.
Hata wote unaowaona kwa social media wenye akaunti kubwa kubwa kwa social media ukiwaangalia profile zao lazima utakuta kuna link ya either website yake au kampuni yake.
Sidhani kama kuna mtu huko mtandaoni yuko serious na kazi yake lakini hana website.
Kujifunza web design na ukaimaster vizuri ni rahisi sana ikiwa tu utapata mtu anayejua na amekuwa akifanya hiko kitu miaka mingi kuliko kukomaa mwenyewe.
Utapita njia fupi ambayo ulitakiwa kujifunza miaka mitatu wewe ukajifunza ndani ya mwezi mmoja au miwili. Hapo unapata muda mwingi wa kutafuta wateja, kufanya kazi za kampuni zinazohusu website.
Pia utaokoa fedha nyingi. Mimi kipindi najifunza web design huko YouTube na kwingine hasa mwaka 2023 pesa ya bundle kwa siku ilikuwa 3k kwa 6k na hapo huna client na unajibana ukipiga kwa mwezi ni 60k+
Vingine nimekuja kuvielewa 2024. Hapa katikati 2023- 2024 kuna pesa nyingi sana imepotea lakini kidogo ukipata wateja ndio mambo yanakaa mkao.
Maisha ya kujifunza mwenyewe ni stressful na pengine usijue mambo kwa kina ila ukipata mtu wa kukufundisha na ukawa serious ni simple sana. Haichukui muda.
Malengo ya kuanzisha tovuti huwa yanatofautiana kulingana na mmiliki wa tovuti hiyo. Malengo yangu na yako yanaweza yakatofautiana kulingana na mitazamo, mahitaji yetu kuwa tofauti
Kimsingi watu wengi wanaoanzisha tovuti huwa na malengo ya kupata pesa. Ukizingatia mabadiliko ya sayansi na technolojia yalivyosaidia kuunganisha watu kuwa kama kijiji, imekuwa rahisi kwa wachache kufedha hizo.
Pale watu walipo ndio pesa ilipo. Kama watu wapo mtandaoni basi pesa zipo mtandaoni.
Tuangalie malengo makuu unayotakiwa kuyangalia kabla ya kuanzisha website yako.
1) Kuuza Bidhaa
Tovuti inasaidia kuuza bidhaa uliyonayo yaweza kuwa ni nguo, vitabu, vifaa vya kielectronic, accessories n.k Hii ndio njia kuu na rahisi wanayoitumia wajasiriamali wengi wa kidigitali.
Wajasirimali wanatumia tovuti kwa ajili ya kuuza bidhaa zao za kimwili au kidigitali. Tovuti inawasaidia kufikia watu kutoka sehemu mbalimbali. Uzuri wake ni kwamba watu wanaweza kununua bidhaa yako kwenye tovuti na kila kitu kikamalizika bila kuonana na mteja.
Kama inavyowasaidia wengine hapa Tanzania hata wewe itakusaidia kutengeneza duka lako mtandaoni na kuuza bidhaa zako. Kuna baadhi ya watanzania wamehamishia maduka yao kwenye website baada ya kuona haiwagharimu sana.
Yeye anahakikisha tu anabundle, ana simu janja basi, kazi iliyobaki ni kuhakikisha atakayenunua bidhaa anafikishiwa bidhaa yake kwa wakati. Ukiwekeza kwa namna hii utashuhudia ukipigiwa simu na wateja ambao huwajawahi kuwafikiria hata siku moja.
Mteja wako anakachokuwa anafanya ni ku-click click tu bidhaa hii hapa. Ikumbukwe: watu hununua bidhaa kutoka kwa watu wanaowajua.
Wewe unataka uanze biashara yako ya kuuza bidhaa kwa njia ya website. Jiulize, watu wanakufahamu? Watu wanaifahamu hiyo website yako, Unafahamika huko mtandaoni? Brand yako ikoje?
Lengo hili huwa ni gumu sana kulifanikisha kama hutotia nguvu na juhudi katika kutangaza bidhaa au huduma unayotamani kuiuza huko kwenye majukwaa mengine ya kidigitali.
Website itakusaidia kufanya mauzo ya bidhaa yako lakini haina uwezo mkubwa wa kuleta watu kwenye hiyo website ukiondoa injini ya utafuta (Search engine). Wewe ndiyo mwenye jukumu la kuleta watu kwenye website hiyo.
Uwezo wako wa kushawishi watu waje kwenye website yako ndio utakaokupa uwezekano wa bidhaa yako kununuliwa. Siyo rahisi lakini inawezekana ukiamua.
2. Tovuti za Washirika (Affiliate websites).
Tovuti hizi huwekwa matangazo ya bidhaa au ya huduma inayotolewa sehemu nyingine. Ulishawahi kutembelea tovuti fulani halafu ukakutana na tangazo linakutaka ubonyeze kisha linakupeleka sehemu nyingine kwenda kununua bidhaa au huduma fulani?
Naam, hizo ndio affiliate websites ninazozizungumzia. Mara nyingi matangazo haya huwekwa kwenye blogs. Mtu anapokuwa anasoma makala fulani ndani yake kuna kuwa na matangazo yanayoonyesha biashara ya mtu mwingine.
Mtu akibonyenza tangazo hilo linampeleka kwenye website inayohusu tangazo hilo. Huko ndo anaweza kufanya kile watengeneza tangazo wamekusudia. Tovuti hizi huwasaidia wenye tovuti kulipwa na kampuni ambalo wamekubali waweke tangazo lao kwenye website zao.
Ikiwa na wewe unataka utengeneza website ya aina hii hauna budi kupata kuwa mwandishi wa makala au kurasa ambazo zitakuwa zinapata watembeleaji wa kutosha.
Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kulipwa ikiwa umetengeneza tovuti yako na inapata watembeleaji wa kutosha 1. Paid per click: Mtu akibonyeza hiyo link (Tangazo) kuna asilimia mmiliki wa tovuti atakulipa. 2. Paid per contract: Mmiliki tovuti (wewe) unaingia mkataba na kampuni inayotaka iweka tangazo lake kwenye website yako.
Kwenye affiliate websites mara nyingi huwa haina faida sana kama huna watembeleza wa kutosha wa tovuti yako. Jinsi unavyokuwa na watembeleaji wengi ndivyo utakavyoongeza nafasi ya kulipwa zaidi kulingana na makubaliano kati yako na mwenye tangazo.
Kama ulishawahi kutembelea tovuti halafu ukakuta kuna matangazo ya BETPAWA sijui BET SASA enhee! Hiyo pia ni aina ya affiliate websites.
3) Kuuza Huduma
Hapa ndipo tovuti hutumika kuongeza ufahamu zaidi juu ya kile mtu au kampuni inakiuza. Naomba tuelewane maana unaweza ukachanganya kati ya huduma na bidhaa.
Huduma inaweza kuwa utengenezaji wa wavuti, hosting services, huduma za ushauri, utoaji wa elimu kuhusu kitu fulani. Mfano: Mimi natoa huduma ya kutengeneza website na kuhost tovuti za watu wengine. Hii siyo bidhaa ni huduma. Mwingine anaweza kusema Graphic designing na mwingine akasema Coaching.
Kwa hiyo tovuti hizi ni kwa ajili ya kuuza huduma uliyonayo. Ukienda thecitizen (Mwananchi) wanatoa huduma ya habari (magazeti), kwa mtu ambaye anataka kuwa anapata taarifa zote basi atalipia kwa mwezi au kwa mwaka ili apewe ruhusu ya kuona kila Habari inayochapishwa.
Unaweza kuamua hata wewe tuseme unatoa elimu kuhusu bima, umuhimu wake, hasara n.k kwa njia ya kozi na ukaifunga kwenye tovuti ili mtu anapotaka kozi hiyo basi aweze kuilipia. Huku ndiko kuuza huduma ninakokumaanisha.
Mtu akikuangalia akaona huna website anaanza kukulianganisha na scams. Sababu biashara nyingi zilizo serious lazima utakuta zina website. Website inayobeba heshima ya biashara zao.
Website inampa mmiliki uwezo wa kufanya kile anachotaka ili kusudi ionekane yakipekee kwenye soko la kidigitali yaani akitaka website iwe na hiki, ifanye hiki, mambo gani aweke kwa namna gani, ni yeye tu.
Leo hii Akaunti zako za mitandao ikifungwa utabaki na nini au biashara yako ndio itakuwa imeshia hapo! Tafakari kisha chukua hatua.
Website ina faida kedekede kama ambavyo nimekuainishia hapa chini.
Uaminifu
Watu siku hizi hawaamini maneno kirahisi rahisi, hawaamini tu kile mtu anapost mtandaoni kwani kumekuwa na watu wengi sana huko mtandaoni wanaosema wanatoa huduma kama yako lakini ukiangalia hawana tovuti/website.
Wengi wanaamini biashara yoyote lazima iliyo serious ina website, wakikusearch halafu wakakukosa wanaanza kukutilia mashaka.
Ni mara ngapi umekuwa ukisikia au ulishawahi kuulizwa, “Je, una tovuti ninayoweza kuangalia zaidi huduma yako?” Siyo kwamba watu hawataki kununua bidhaa au kupata huduma yako! Hapana.
Wanataka kupata ushahidi na maelezo zaidi kwamba ni kweli unaweza kutimiza ahadi zako unazoahidi huko mtandaoni. Isije ukawaingiza chaka.
Ujue kila mtu anaweza kutengeneza akaunti Twitter (X), LinkedIn au Instangram lakini ni wachache wanaoweza kutengeneza website. Kuwa na website ni ishara ya kuwa wewe ni mwaminifu ndiyo maana watu huuliza una website?
Kuwa na website ni zaidi ya kuwepo mtandaoni—ni pamoja na kukujengea uaminifu wako katika enzi hizi za kidijitali. Inakuonyesha kwa wateja wako kuwa upo serios na biashara, kweli umewekeza katika biashara yako.
Bila website watu watakuwa wanakuangalia tu huko mtandaoni, utakuwa unapoteza fursa nyingi zinaenda kwa washindani wako ambao tayari wana website kali.
Tovuti/website hailali wala haichukui likizo. Ipo hewani masaa 24 ikikutangazia biashara yako. Ikiwa website imetengeneza kitaalamu, yenye mvuto, yenye maneno ya ushawishi ndani yake inaweza kukupatia faida mara dufu ndani ya muda mchache.
Website ni kwa ajili ya kuuza/kutangaza huduma yako
Shida ya makampuni mengi yanatengeneza website ili yaonekane yana website. Je hilo ndilo lengo! Website ni kwaajili ya kutangaza, kukuza biashara kisha ikupatie wateja watakaokulipa ili uwapatie huduma yako.
Usiruhusu website yako ikae tu kama haipo. Tengeneza tovuti itakayokupatia faida itakayoonyesha kazi zako, itakayotoa ushuhuda (wateja uliowahi kuwasaidia).
Imarisha uaminifu wako mtandaoni na sifa zako leo kwa njia ya website.
Tengeneza tovuti inayothibitisha unaweza kufanya unachosema, na uone jinsi inavyogeuka kuwa chombo chako cha thamani zaidi cha masoko mtandaoni.
Changamoto nyingine ambayo watu huwa wanakuja kulaumu kuwa website haisaidii. Unatengeneza website halafu huipromote yaani huitangazi kwenye mitandao ya kijamii muda huo huo unataka watu wengi waitembelee na upate wateja wengi kweli!
Website ndiyo makao makuu ya marketing ukitengeneza website isemee kwenye mitandao hivyo ndivyo unavyojitangaza na kuvutia wateja.
Mtu atayetengeneza website atafanya upate wake ionekane kwenye search engine pale mtu anaposearch kitu mtandao basi website yako ipate kupendekezwa ionekana. Pia na wewe ufanye upande wako.
Website ni utambulisho wako mkubwa mtandaoni
Website itawafanya hata watu ambao walikuwa hawakujui wakujue kwa undani kwa muda mchache. Kuliko ile mtu aanze kuscroll kwenye social media akaunti zako halafu ndo akute huo mda ulikuwa unapost mambo unayoyajua mwenyewe unafikiri.
Ataendelea kukufuatilia? Kwenye mitandao ya kijamii unaweza kupost chochote ili uchangamane na watu wengine lakini kwenye website content zinazokaa pale ni zile za muhimu tu.
Yaani ni rahisi mtu kukupa umakini zaidi hata kumfanya akupigie simu kwa majadiliano zaidi.
Jarida la leo nchini marekani –Top website statistics you should know in 2024linasema takribani website mpya 252,000 zimekuwa zikitengenezwa kila iitwapo leo ambayo ni sawa na kusema website 10,500 zinatengenezwa kila lisaa au website 3 kila sekunde.
Hii ina maanisha ni kwa jinsi gani website zimekuwa zikifaidisha wafanya biashara wengi. Hasa wafanya biashara wanaotamani kupanua na kutangaza biashara zao mtandaoni.
Ukitaka kutengeneza website kali itakayokutangaza vizuri kwenye digitali hakikisha unaangalia na kampuni, agency, developer au designer anayeelewa fikra za wateja wako nikimaanisha saikolojia ya website development.
Siku moja nilikuwa nimekaa zangu ghetto mida ya saa kumi na mbili jioni nasoma Hekaya za Abunuwasi, ghafla ujumbe ukatumwa kupitia WhatsApp kutoka kwa rafiki yangu akisema nimsaidie kutangaza hard disc drive aliyokuwa anauza.
Bila hiana kesho yake nikaipost kwenye status yangu, wakati huo sina uhakika kama kuna mtu anaweza kuinunua lakini baada ya muda mfupi habari njema zikaanza kuonekana kwenye whatsApp chat, maswali yakawa mengi wadau wanauliza bei na kupita hivi.
Bahati nzuri kuna jamaa mmoja kweli alikuwa anahitaji hard disc kwa sababu compyuta yake ilikuwa na space ndogo so akanifuata DM na hatimae aliinunua hiyo disc kutoka kwa jamaa yangu baada ya kumpa maelekezo.
Tangu siku hiyo, fikra zangu kuhusu WhatsApp zilibadilika kabisa nikajisemea moyoni “Kumbe WhatsApp inaweza kuwa iko vizuri zaidi kuliko Twitter na Instagram!” Kwamba kupitia status unaweza kuuza kitu chochote na watu wakanunua.
Unapataje wateja?
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali hata mimi nilikuwa sina imani saana kama hiyo Hard Disk inaweza kununuliwa ila kitu nilichojifunza ni kuwa mteja ni yeyote yule anayeweza kuona status zako. Mtu yeyote mwenye uwezo wa kuona status yako huyo ni mteja. Anaweza asiwe mteja wako wa moja kwa moja lakini akawa na marafiki zake wanaohitaji bidhaa unayouza.
Kuna uwezekano mkubwa wa kutokuuza ujuzi ulionao au kupata mteja papo hapo. Yaweza kuchukua wiki au miezi ndo unaanza kupata wateja hao. Siku moja nilikuwa napiga story na jamaa yangu anaitwa kastory wengi wanamfahamu kama Castroelectronics alisema “Huwezi amini mwanangu vitu vyangu vingi huwa nauza kupitia status”.
Haikugharimu chochote kupost vitu unavyouza kwenye WhatsApp status yako. Unajua vijana wengi tunaogopa kujulikana kuwa tunafanya biashara fulani ndo mana huwa hatupost chochote ni meme mwanzo mwisho.
Haya ni maisha yako unamwogopa nani, unahofia nini. Halafu ukumbuke kuishi kwa kuangalia watu wengine watasemaje, watakuonaje ni sawa na kujichimbia shimo la umauti. Ulizaliwa peke yako utakwenda peke yako. WhatsApp ni fursa moja nzuri ambayo wachache wanaojua kuitumia vizuri wanafaidika sana.
WhatsApp Channel na WhatsApp Group.
Kabla ya kuongezwa kwa WhatsApp channel feature wengi walikuwa wanatumia whatsapp group kuendesha shughuli zao mbali mbali ikiwemo uelimishaji, seminas, kupashana habari pamoja na kufanya biashara zao huko.
Lakini kila kukicha mambo mapya yanaibuliwa leo hii tuna WhatsApp Channel inayokupa fursa ya kuwafikia mamilioni ya watu wanaokadiliwa kuwa ni 2.78billion na wanazidi kuongezeka kila siku.
Wataalamu wanasema channel zote hupewa kipaumbele cha kuonekana kwa mtu yeyote anayetumia WhatsApp kwa sababu by default iko public, yeyote anaweza kufollow channel hiyo. Nadhani ulishawahi kuziona kwenye whatsapp yako kama ambavyo zinaonekana kwangu hapa. Vivyo hivyo hata channel utakayotengeneza itapewa upendeleo huo.
Jinsi ya kutengeneza WhatsApp Channel
Kutengeneza WhatsApp chanel siyo kazi ngumu, ni rahisi kabisa fanya kufungua application yako ya WhatsApp, nenda kwenye updates
Angalia kuna alama ya kujumuisha ibonyeze.
Bonyeza Create channel.
Click continue
Upload profile picture, Andika jina la channel pamoja na maelezo mafupi kuhusu hiyo channel yako yaani biashara yako inahusu nini (kwa ufupi).
Bonyeza Create Channel.
Hapo utakuwa tayari umeshatengeneza WhatsApp channel kinachofuata ni wewe kuendeleza channel yako.
Jinsi ya kutafuta fursa za kazi kupitia WhatsApp.
Ikiwa bado unatafuta kazi au bado ni mwanafunzi, whatsapp ni sehemu nzuri ya kutangaza na kuonyesha uwezo ulionao juu ya kazi fulani. Rafiki yangu mmoja anasoma Arusha Tech niliwahi kumwambia “The best place for you to find jobs is WhatsApp“. Akasema “Anthony, unajua sijakuelewa vizuri“.
Ikabidi nimweleweshe. Leo hiii tunaongea mimi na wewe tuko hapa Arusha kesho na kesho kutwa huenda wewe ukapata kazi huko Itaba na katika hiyo kampuni akawa anahitajika website developer. Ukizingatia wewe ndo upo incharge ukitizama nani anaweza kufanya hiyo kazi huoni si utanipigia simu mimi ambaye ulikuwa unaona status zangu?
Je vipi kama ungekuwa unaona napost tu memes kila siku ungejua kama naweza kutengeneza website? Ungenipigia simu ili nichangamkie hiyo fursa? Naam naamini umenipata. No one knows tommorow.
Fursa haziji ukiwa umelala. Nakumbuka pia siku za nyuma hapo nilikuwa nashiriki kwenye mijadala kwenye magroup ya watu wengine nilijitahidi kutoa mchango wangu kulingana na uelewa wangu kuhusu mada walizokuwa wanazungumzia na uhalisia wa mambo yalivyo, pale walipoenenda tofauti niliwaambia.
Kwa sababu nilijua hii ni fursa ya kuwekeza jina langu miongoni mwa watu.
Aisee kama unajua unajua tu ilikuwa saa nne usiku kiongozi wa hilo group akanitumia ujumbe kama unavyosomeka hapo chini.
Mtu akianza kukutafuta kwa njia kama hivi ujue kuna kazi umefanya. Hizi ndiyo connection. Unatangaza na kukuza jina kwa style kama hii.
Ninachotaka kusema ni kwamba fursa za kazi zinaweza kupatikana sehemu yoyote ile siyo lazima uende kuomba kazi maofisini hata kupitia whatsApp unaweza kufanikisha hili. Kuna kitabu kimoja nilikuwa nasoma kinaitwa “Mbele Ya Muda” kimeandikwa na Shukuru Amos, anasema kazi yake ya kwanza ilitokana na watu kuona makala zake ambazo pia alikuwa anazipost kwenye status yake.
Hao hao watu unaobonga nao, wanaoona staus zako kila siku wanaweza wakakurecommend sehemu kutokana na vitu ambavyo huwa unashare.
Watu hatufanani leo hii mko wote sawa. Kesho mwenzako manager wewe mtafuta ajira kwa hiyo siku moja historia inaweza kukubeba manager kaona kuna kazi uwezekano wa kukujulisha au kukuita ni mkubwa kwa sababu alishawahi kuona mambo unayofanya.
Sasa vipi kama ungekuwa unaongea pointless tu ukiwa na wenzako. Je, unaweza kweli ukaitwa kwa style hiyo? Hapana huwezi.
Chukulia hiyo ndiyo fursa ya kujitangaza na kuonyesha umahili wako huwezi kujua huko mbeleni mambo yanaweza kuwaje. Kuwa serious hiyo ni fursa itumie vizuri.
Kupitia WhatsApp status.
Nimesema, vijana hasa wale wanaosoma huwa hawataki kuonyesha kile wanachokijua. Utakuta kwenye status ameweka memes mwanzo mwisho, picha zao mwanzo mwisho, vichekesho mwanzo mwisho yaani hakuna hata kiashiria kinachoonyesha ujuzi wao.
Siyo mbaya lakini kitu cha kujiuliza ni kuwa unaacha nini kwenye vichwa vya waangaliaji wa status zako. Mtu akiangalia status zako mbili tatu kitu gani atabaki nacho kichwani kuhusu wewe?.
Kama kweli unataka kutafuta kazi kupitia WhatsApp jaribu angalau kuwa open kwenye status zako sema ni nini unajua, unafanyaje na unaweza kumsaidia nani.
Unaweza usione matokea kwa muda huo lakini baada ya muda utaanza kutafutwa. Hili nina uhakika nalo usimdharau mtu kwa kuangalia hadhi aliyonayo leo.
Yote kwa yote mchukulie mtu anaeangalia status zako kama mwajiri wako wa baadae. Jiamini na career yako hata kama hutakuja kuwa huyo uliye leo naamini kuna kitu lazima utajifunza.
Mwisho.
Suala la kusaka tonge mara nyingi huwa ni gumu lakini WhatsApp siku moja inaweza kubadilisha maisha yako. Maamuzi yako leo ndiyo matokeo ya kesho. Uwe na siku njema.